Ni Muda Muafaka Kwa BeyHive Kuwa Tayari Kumpokea Malkia Wao. Taarifa kutoka mitandao mbalimbali zinasema kuwa Byeonce Ammepanga Kuyaweka Hadharani Maisha Yake Kupitia Documentari Itakayoelezea Kila Kitu Kumuhusu Yeye Kwa Kipindi Cha Miaka Miwili Iliyopita.
Taarifa Iliyoripotiwa Na Mtandao Wa Vibe Inasema Kuwa, Documentari Hiyo Itaanika Tour Yote Ya Lemonade Album Iliyojulikana kama Formation Tour. Taarifa Zinaendelea Kusema Kuwa Queen Bey Yupo Katika Mazungumzo Ili Kuyaweka Maisha Yake Hadharani Na Pia Hata Ule Usiri Juu Ya Mimba Ya Mapacha Wake Beyonce Nao Utawekwa Hadharani Kupitia Documentari Hiyo.
Mpaka Sasa Haijajulikana Documenatry Hiyo Itarushwa Kupita Kituo Kipi Cha Television Japo Bado Kuna Mapambano Ya Kibiashara Kati Ya Netfix Na HBO. Mshindi Kati Ya Watemi Hawa Ndiyo Atapewa Nafasi Ya Kuyaanika Maisha Ya Queen Bey Hewani.
Katika Documentari Hiyo Tutarajie Kuyaona Majina Ya Mastar Kibao Wakiwemo Jay Z, Kendrick Lamar, Serena Williams Na Wengine Kibao
Our EXCLUSIVE on Beyoncé's upcoming Documentary, the bidding war between HBO and Netflix & The Formation World Tour! 🐝🔥 pic.twitter.com/ZS1lja3ZRP— THE BEYHIVÉ (@TheBeyHiveTeam) July 28, 2017
0 comments:
Post a Comment