Celebrity

Jaden Smith Awajibu Wanaopiga Vita Mavazi Yake

 
Kumekuwa Na Mashaka Sana Hasa Juu Ya Muonekano Wa Jaden Smith Kutokana Na Mavazi Yake Ambayo Amekuwa Akivaa Siku Za Hivi Karibuni.

Jadeni Amekuwa Akivaa Mavazi Yanayoonekana Kuwa Kama Ya Kike Kitu Ambacho Kimekuwa Kikizungumzwa Mnoo Katika Mitandao Ya Kijamii.

Jaden Anayetegemea Kutokea Katika Ukurasa Wa Juu Wa Jarida La Nylon Kwa Mwezi Wa Nane, Amesema Haya Baada Ya Kuulizwa Juu Ya Upinzani Anaoupata Kutoka Katika Jamii Mbalimbali.

Jaden Alisema "Unachotakiwa Kufanya Ni Kujiamini Wewe Mwenyewe" Katika Kuwekea Msisitizo Jaden Aliongeza "Dunia Itaendelea Kunipinga Juu Ya Kile Ninachokifanya, Lakini Nitaendelea Kutokujali, Nitaendelea Kufanya Hiki Hiki, Na Nitafanya Mengi Zaidi  Kama Haya"

Jaden Anaamini Kile Anachokifanya Leo Kitakuja Kusadia Wengine Huko Mbeleni, Alisisitiza Hilo Kwa Kusema "Miaka Mitano Ijayo Kijana Akiamua Kwenda Shule Amevaa Sketi, Wenzake Hawatamcheka.

Nafanya Haya Ili Kusaidia Watoto Wangu Na Watoto Wa Uzao Ujao, Nataka Kuona Vizazi Vijavyo Vione Kuwa Vitu Vingine Ni Vya Kawaida Sana Japo Vilikuwa Havikubaliwi Katika Jamii Yangu"

Jaden Aliongeza Kwa Kusema "Nadhani Watu Wanashindwa Kuelewa Maana Ya Jinsia, Sisemi Kuwa Nafahamu Hilo, Ila Ninachotaka Kusema Ni Kuwa Sioni Tofauti, Sioni Tofauti Ya Nguo Za Kike Na Nguo Za Kiume, Ila Ninavyokiona Ni Kuna Watu Waoga Na Wale Wanaojiamini" Alimaliza Jaden

Vipi Wewe Unasemaje Je Yuko Sahihi? Upo Tayari Kuona Mwanao Wa Kiume Akivaa Sketi? Dondosha Maoni Yako Hapa Chini

About TNZ: Entertainment News

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.