Ukuaji Wa Teknolojia Unasababisha Uvumbuzi Wa Mambo Mengi Ambayo Yanaweza Kuwa Faida Kwa Binadamu au Wakati Mwingine Hata Kuleta Hasara Kwa Binadamu.
2007- Lucy Baada Ya Kuchukua Nafasi Ya Ukuu Wa Kampuni Ya Mirando Corporation, Anafanikiwa Kugawa Mbegu Za Nguruwe Katika Maeneo Mbalimbali Ambao Watakuwa Wanafugwa Katika Mashamba Yanayomilikiwa Na Mirando Corporation.
Lengo La Kutawanya Mbegu Hiyo Ya Nguruwe Ni Kushindanisha Wafugaji Hao Na Miaka 10 Baadaye Atatangazwa Mshindi. Mshindi Ni Yule Ambaye Atakuwa Amemfuga Na Kumfanya Nguruwe Huyo Kuwa Mkubwa Kuliko Wote.
Miaka 10 Baadaye Katikati Ya Milima Nje Kidogo Ya Mji Wa Seoul Huko Korea Kusini, Anaonekana Binti Mdogo Anayejukalikana Kama Mija. Mija Ndiye Aliyekuwa Mwangalizi Wa Nguruwe Mkubwa Anayeitwa Okja Akisaidiana Na Babu Yake.
Muda Wa Kumtangaza Mshindi Wa Shindano La Ufugaji Unakaribia Na Kupitia Mtaalamu Wa Mifugo Wa Mirando Corporation Dr John Anawasili Katika Milima Hiyo Ya Korea Kusini Na Kushangaa Kumona Nguruwe Mkubwa Kuliko Wote Na Anatangazwa Mshindi.
Mija Akiwa Haelewi Kinachoendelea Anarudi Anakuta Banda La Okja Lipo Wazi Na Okja Hayupo Anamuuliza Babu Yake, Babu Anamwabia Okja Ameshinda Hivyo Amechukuliwa Na Anapelekwa New York. Ni Kitu Ambacho Alikuwa Hakitaki Kitokee, Mtoto Mija Anaamua Kwenda Seoul Kupambana Ili Kumbakisha Okja Katika Himaya Yake. Hakutaka Kumpoteza Kabisa Okja.
TRAILER
Akiwa Seoul Anagundua Kuwa Okja Anaenda Kuuliwa Na Kutengenezewa Soseji. Kwa Msaada Wa Kundi Linalojiita ALF Mija Anafanikiwa Kumpata Okja. Wakiwa Kwenye Gari Mija Akiwa Haelewi Kinachoendelea Kiongozi Wa Kundi La ALF Anajaribu Kumshawishi Mija Akubali Kumuachia Okja Aende New York. Kwa Kuwa Kiongozi Huyu Haelewi Kikorea Anamtumia Mkalimani Kuwasiliana Na Mija. Mija Anakataa Kabisa Kumpeleka Okja New York Pamoja Na Kupewa Ahadi Kuwa Wao ALF Watamuokoa Kwani Wanataka Kumtumia Okja Kama Chambo Ya Kuanika Uovu Wa Kampuni Ya Mirando Corporation.
Mija Anakataa Kabisa Lakini Yule Mkalimani Anawaambia Kuwa Mija Amekubali Okja Apelekwe New York. Mija Anashindwa Lakini Hakati Tamaa Anamua Na Yeye Kwenda New York.
Unaweza Kuidownload Hapa
Usisahau Kutuachia Comment Yako Hapa Chini
0 comments:
Post a Comment