Movies

Emirates Walivyofanikisha kuionesha Despicable Me 3 Mlimani City


Jumamosi Ya Tarehe 8/7/2017 Ilikuwa Ni Siku Ya Furaha Kwa Watoto Wa Dar es Salaam Baada Kushuhudia Filamu Ya Despicable Me 3. Filamu Hii Ambayo Ni Animation Iliangalia Na Watoto Zaidi Ya 30 Wakiwa Wamesindikizwa Na Wazazi/Walezi Wao. Kampuni Ya Usafirishaji Wa Anga Ya Emirates Wakiwa Ndiyo Wenyeji Wa Shughuli Hii


Wazazi Na Watoto Wakifurahia Sinema Ya Despicable Me 3

Hafla Hii Fupi Ilifuatiwa Na Chakula Cha Mchana Kwa Wageni Wote Chini Ya Usimamizi Wa Emirates. Akiongea Na Wazazi Hao Mkurugenzi Mkuu Wa Emirates Tanzania Bw. Rashed Alfajeer Alikuwa Na Haya Ya Kusema " Emirates Ipo kwa Ajili Ya Kutoa Thamani Kwa Pesa Na Wamejihakikisha Kutoa Huduma Iliyo Bora Angani Mpaka Ardhini Na Hakuna Tofauti Linapokuja Suala La Familia Katika Kusafiri. Kwa Watoto, Lazima Wawekwe Huru Na Waburudike Na Kuwajali Kwa Kuwapa Wigo Mpana Katika Kuchagua Sinema Na Programu Ili Kukithi Mahitaji Yao. 


Mkurugenzi Wa Emirates Tanzania Bwana Rashed Alfajeer Akizungumza Na Wazazi na Watoto

Pia Katika Hafla Hiyo Bwana Rashed Alitangaza Ofa Kwa Wanafamilia Wanaotaka Kusafiri Katika Nchi Mbalimbali Duniani Kuwa Emirates Pia Ilipata Uzoefu Wa Familia Katika Kutangaza Ofa Ya 50% Katika Daraja La Uchumi Kati Ya Abiria 2 - 8 Kusafiri Wote Katika Sehemu 21 Zilizopendekezwa Kama Uarabuni, Ulaya Vile Vile Marekani Kusini Na Kaskazini. Hiyo Ofa Ni Kati Ya Tarehe 6 Na 14 Julai 2017 Na Za Nje Kati Ya Tarehe 6 Julai Na 10 Disemba 2017.

Ofa Hii Maalum Inatoa Nafasi Kubwa Kwa Familia Kuwa Na Likizo Ya Pamoja Sehemu Mbali Mbali Kwa Gharama Nafuu Kwa Muda Uliowekwa Tu Na Kuongeza Wakati Wakisafiria Na Emirates, Familia Itarajie Kupata Wigo Mpana Wa Program Za Watoto Ikiwa Na Channeli 90 Mahususi Kwa Ajili Ya Kuwaburudisha Watoto Ikiwamo Pamoja Na Sinema Bora Na Programu Za TV Kutoka Disney, Cartoon Network, Cbeebies Na Nickelodon Na Nyingine Nyingi. Chakula Pia Upewa Kipaumbele Sana Pindi Abiria Wawapo Angani Kwenye Emirates. Watoto Wenye Umri Kati Ya Miaka 2 Na 12 Hupewa Chakula Maalum Wakihudumiwa Katika Vyombo Vya Kisasa Wakiwa Na Staff Pamoja Na Marubani. Wasafiri Wenye Ugunduzi Wachache Wanaweza Kupata Marafiki Wapya Pindi Wawapo Safarini, Kuna Blanketi Kwa Ajili Ya Kujifunika Na Kuweza Kujiburudisha Na Majarida Yanayokuja Dar Es Salaam Kila Siku. Ndege Ya EK 0725 Inatoka Dubai Saa 10:25 Na Kufika Dar Es Salaam Saa 14:50. Ndege Inayorudi EK 0726 Inatoka Dar Es Salaam Saa 16:45 Na Kufika Dubai Saa 23:20.

Tumekuwekea Hapa Trailer Ya Sinema Hii

About TNZ: Entertainment News

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.