Celebrity

Umri Ndiyo Sababu Ya Kuachana Na Kylie - Tyga


Uhusiano Wao Ulikuwa Ni Moja Ya Habari Zilizoandikwa Sana Duniani. Umaarufu Ukaaongezeka Zaidi Na Dili Za Kutunisha Mfuko Zikaja Za Kutosha. Moja Ya Dili Iliyoshangaza Ni Ile Ya Sex Tape. Na Inasemekana Walifanya Hiyo Sex Tape Japo Juzi Kylie Alisisitiza Hata Dunia Ifanye Vipi Sex Tape Haitokuwa Hewani.

Katikati Ya Mwezi Wa Tano Wawili Hao Wakasema Basi Kuwa Pamoja Acha Kila Mtu Afanye Mishe Zake. Akiongea Na Bigboy TV Tyga Aliweka Wazi Moja Vitu Vilivyochangia Wawili Hao Kuachana.

Kwa Mujibu Wa Tyga Anasema Umri Pamoja Na Umaarufu Wa Kylie Ilikuwa Ni Moja Ya Vitu Vilivyasababisha Mapenzi Yao Kuota Mbawa.

Tyga Alisisita "Unapokuwa Na Mapenzi Ya Namna Ile (Mapenzi Ya Wazi Na Umaarufu) Ni Vigumu Sana Jamii Kukuona Tofauti Na Vile. Mapenzi Yale Yamechukua Kila Kitu Changu, Kikazi Yamechukua Kila Kitu Nilichopigana Kukipata"

Tyga Anasisitiza Kuwa Yeye Na Jenner Bado Marafiki Tena Sana Na Bado Anaamini Wanaweza Kurudiana Hapo Baadaye. Tyga Alisema "Unapokuwa Bado Kijana Mdogo Kuna Makosa Ambayo Huwa Unafanya. Na Makosa Haya Yanakuwa Ndiyo Habari Katika Jamii, Hii Ni Hatari Na Huweza Kuweka Mapenzi Yenu Mahali Pabaya. Ila Kwa Nataka Kurudi Katika Hali Yangu Ya Awali. Nataka Kumrudisha Tyga Wa Awali Lakini Bado Namfikiria Kylie Sana"

Tyga Anaongeza Kuwa Kuachana Kwao Hakukuwa NA Ugomvi "Ilifikia Kipindi Tukasema Tuheshimiane, Nikuheshimu Na Wewe Uniheshimu, Ni Maamuzi Mzuri Kwa Pande Zote. Pale Mambo Yanapokuwa Hayaendi Sawa Inabidi Ujipe Nafasi Ya Kurekebisha, Tuliamua Kila Mmoja Kujipa Muda"

Tumekuwekea Interview Yote Hapa Chini

About TNZ: Entertainment News

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.