Series

New Season, Kali Zilizorudi Hewani


Baada ya Kutuonjesha Kwa Uhondo Wa Aina Yake Kisha Wakaenda Mapumziko Sasa Wameamua Kurudi Tena Hewani Kutupatia Kile Kitu Roho Inapenda.

Yes, Series Kadhaa Zilikuwa Mapumzikoni Huku Wakijiandaa Na Mizigo Mipya Ili Kukonga Nyoyo Za Mashabiki. Sasa Mapumziko Yameisha Ni Bampa To Bampa Tunaanza Kuzihesabu Episodes Mpya Mpaka Tumalize Season Nzima.

Queen Of The South.
Moja ya Series Zilizokuwa Zinasubiriwa Kwa Hamu Ni Hii. Mwanamke Anafanya Kazi Chini Ya Madrug Lord Wawili, Baada ya Kuzijua Mbinu Zote Wanazotumia Sasa Anachoka Kuwa Mtumwa Anahitaji Kujenga Empire Yake, Ili Awe Queen, Yes Queen Of The South. Hujaiona? Basi Unapitwa Na Vizuri Vingi Season Ilitoka na Tukafaidi Epsode 13 Zilizoshiba Sasa Wamekuja Na Season 2, Hebu Fanya Kuitafuta Ili Tufurahi Pamoja.

Dark Matter
Unapenda SCI-FI Series? Basi Huu Ni Mzigo Unaotakiwa Kuwa Katika Libary Yako. Tumeshahesabu Season Mbili Na Ya Tatu Ndiyo Kwanza Tumeianza. Pale Washkaji Wanapoamka Na Kujikuta Wasipokujua Pia Hawana Kumbukumu Kuhusu Wao na Hata Majina Yao Hawayakumbi, Wanaamua Kuungana Na Kuhakikisha Wanapambana na Kila Baya Linalokuja. Kuna Siri Kubwa Sana Juu Ya Kumbukumbu Zao, Wanaamua Kuutafuta Ukweli Kwa Hali Na Mali. Swali Je, Watakuwa Tayari Kuupokea Ukweli Juu Yao? 


Fear the Walking Dead
Hii Ni Spin Off Ya The Walking Dead, Nilishawahi Kuieleza Kwa Kirefu Sana Katika Insta Page Yangu. Jumla Ya Epsodes 23 Zikiwa Zimesharuka Hewani, S01 Ikiwa Na Episodes 6, Huku S02 Imebeba Mzigo Wa Episodes 15, Na S03 Ndiyo Kwanza Imesharusha Epsodes 2 Kati ya 16 Zinazotarajia Kuruka. Hii Ni Moja Kati Ya Horror Movies Ambayo Inastahili Kuwa Katika Library Yako. 


Nyingine Ambazo Zimeruka Mpaka Sasa Ni
Sunday, June 4
I’m Dying Up Here (Showtime, 10 p.m.)
Monday, June 5
Stitchers (Freeform, 9 p.m.)
Thursday, June 8
Queen of the South (USA, 10 p.m.)
Friday, June 9
Dark Matter (Syfy, 8 p.m.)
Wynonna Earp (Syfy, 10 p.m.)
Saturday, June 10
Orphan Black (BBC America, 10 p.m.)
Idiotsitter (Comedy Central, 8 p.m.)


Wale Wa Power Tukutane 25 June.

About TNZ: Entertainment News

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.