Ulimwengu Wa Burudani Umeshikilia na Kelele Na Majigambo Ya Wapenzi Wa Burudani Wenyewe. Zile Kelele Za Mashabiki Ndiyo Hasa Huwapa Hamasa Watumbuizaji Kutafuta Namna Nzuri Ya Kuweza Kuwakutanisha Mashabiki Hao.
Kila Celebrity Yuko Na Staili Tofauti Ya Kuwakutanisha Mashabiki na Kuwa Karibu Na Mashabiki Hao. Utafauti Huu Ndiyo Msingi Wa Kuwa Na Identiy Kati Ya Mashabiki Wa Msanii Fulani na Msanii Mwingine. Hapo Ndipo Kunapozaliwa Makundi Mbalimbali Yanayokuwa Supported Na Wasanii Hawa
Hukuo Ndiko Kulisababisha Kuzaliwa Kwa Makundi Kama Beliebers, Rihanna Navy, BeyHive, Team Breezy, Na Hata J.lovers.
Tumekukusanyia Majina Ya Mashabiki Wa Mastaa Mbalimbali Duniani. Ukimaliza Kusoma Usisahau Kutuachia Comment Chini Na Kutuambia Kuwa Na Wewe Ni Timu
Rihanna Navy: Rihanna
Moja ya Kundi Ambalo Lina Nguvu Sana Katika Ulimwengu Wa Burudani. Rihanna Navy Wako Tayari Kufanya Lolote Lile Hasa Linapokuja Suala La Kipenzi Chao Rihanna. Movie Ya Battleship Ambayo Rihanna Alicheza Kama Navy Ndiyo Nguzo ya Kuzaliwa Kwa The Navy. Navy Ya Rihanna Imeendelea Kukuwa Kwa Kasi Sana Huku Ikiungwa Mkono Na Rihanna Mwenyewe Na Tafiti Zinasema Rihanna Ni Miongoni Mwa Watu Maarufu Wachache Wanaoheshimu Na Kutambua Umuhimu Wa Mashabiki. Kupitia Hilo Rihanna Amekuwa Karibu Sana Na Mashabiki Wake Na Amekuwa Akiwafatilia na Kuwafurahisha Kupitia Sauti Na Tungo Za Nyimbo Zake.
Beliebers: Justine Beiber
Kutoka Katika Jina Lake La Beiber Na Neno Believe Ndipo Likazaliwa Jina Beliebers. Hii Muunganiko Wa Mashabiki Wa Kijana Machachari Kutoka Canada Anayefanya Muziki Wake Marekani. Justine Beiber Ndiye Nguzo Ya Beliebers Akiwaunganisha Mashabiki Wote Duniani Kupitia Muziki Wake Kwa Nembo Moja tu Ya Beliebers
Bey Hive: Beyonce
Moja Ya Kundi Lenye Nguvu Na Mapenzi Ya Kutosha Kwa Beyonce, Ukitaka Kuiona Dunia Chungu Hebu Jaribu Kusema Vibaya Beyonce, Utajua Hasa Nini Maana Ya Fan Base Kupitia Bey Hive. Bey Hive Wanasemwa Kuwa Ni Moja Ya Makundi Machache Sana Ya Ubunifu Wa Hali Ya Juu, Ubunifu Huo Ndiyo Unaendelea Kumfanya Beyonce Kuwa Juu. Wenyewe Bey Hive Wanapenda Kumuita Beyonce "Queen Bey"
Swifties: Taylor Swift
Wakati Anaanza Muziki Watu Hawakufikiria Kama Ataliteka Soko Kwa Haraka Kama Alivyofanya, Akiwa Amejiwekea Rekodi Za Aina Yake Zikiwemo Tuzo Ya Album Bora Ya Mwaka Katika Tuzo Za Grammy Na Kumfanya Kuwa Mwanamuzi Wa Kwanza Mwenye Umri Mdogo Kushinda Tuzo Hiyo Akiwa Na Miaka 2o Tu. Aliendelea Kutengeneza Hit Song Na Haikuchukua Muda Akawaamejiwekea Nafasi Ya Pekee Katika Mioyo Ya Wapenda Muziki. Neno Swifties Likonyofolewa Kwenye Jina Lake Na Kutengeneza Himaya Ya Die Hard Fans Wa Taylor Swift
Directioners: One Direction
Ulimwengu Wa Burudani Ulifurahia Nyimbo Nyingi Za Hisia Kutoka Kwa Vijana Watano Waliounda Kundi La One Direction. Popote Walipokwenda Lazima Walipokewa Vizuri Na Mashabiki Wao. Kwa Sababu Ya Jina Lao Kuwa Ni Direction Basi Wakaona Itakuwa Busara Kuwapa Jina La Directioner Wale Wanaowafanya Kuwa Hapo. Kwa Sasa Wamepumzika Kuimba Kama Kundi Ila Wameahidi Kurudi Stronger, Lakini Directioners Bado Wapo Kote Duniani Na Bado Wanaendelea Kufurahia Nyimbo Nzuri Zilizonakshia Na Sauti Za Kipekee Kutoka Kwa One Direction
Team Breezy: Chris Brown
Kutoka Katika Nickname Ya Breezy Inayotumiwa Na Chris Brown Ndipo Ilipozaliwa Team Breezy. Kama Hujui Maana Ya Royal Fans Basi Iangalie Hii Team, Wamekuwa Nyuma Na Kuendelea Kumsupport Kipenzi Cha Hata Pale Anapopatwa Na Majanga. Mwenyewe Chris Brown Amewahi Kusema Hana Namna Nzuri Ya Kuwashukuru Team Breezy Kwa Kuendelea Kumshika Mkono Hata Pale Anapoteleza.
Lambs: Mariah Carey
Hajabarikiwa Sauti Tu Ya Kuwaunganisha Wapenda Muziki Duniani. Ni Raha Sana Kumsikiliza Akiimba Live Au Hata Kwenye CD, Inawezekana Kabisa Sauti Yake Nzuri Ndiyo Ikawa Sababu Ya Kuendelea Kuwa Na Watu Lukuki Wanaendelea Kumpa Support. Mwaka 2012 Aliifanya tarehe 11 February Kuwa Ni Siku Ya Mashabiki Wake Wote.
Selenators : Selena Gomez
Anaigiza, Anaimba Anawathamini Mno Mashabiki, Anaamini Mashabiki Wake Ndiyo Nguzo Ya Mafanikio Yake. Na Neno Selenator Wachambuzi Wa Masuala Ya Burudani Wanasema Linaweza Kufananishwa Na Terminator Yaani Nguvu Na Uwezo. Na Selena Kwa Kuonesha Kuwa Anawathamini Mashabiki Wake Alishawahi Kubuni Mavazi Yenye Jina Lao La Selenator, Unaweza Kucheki Katika Account Yake Ya Instagram.
Lovatics: Demi Lovato
Umewahi Kuisikia au Kuisoma Urban Dictionary? Kama Bado Basi Itafute Na Itakupa Maana Ya Majina Mbalimbali Ya Fanbase. Katika Dictionary Hii Wanaamini Kuwa Kuna Tofauti Kubwa Sana Kati Ya Shabiki Wa Demi Lovato na Lovatic. Wanaamini Siyo Kila Shabiki Wa Demi Lovato Anaweza Kuwa Lovatic.
Wao Wanasema Kuwa Lovatic Ni Yule Mtu Anayempenda Demi Lovato Pamoja Na Mapungufu Yake Kama Inavyosomeka Katika Dictionary Hiyo "Lovatic is that one person who supports her, no matter what. Lovatic is that one person who doesn’t leave her because she is not perfect, but loves her even more because of her flaws. Lovatic is an f—-g SKYSCRAPER" Unaweza Ukasoma Zaidi Hapa
KatyCats: Kate Perry
Kupitia Tour Yake Ya "Hello Katy" Ndipo KatyCats Ikatambulisha Duniani. Pamoja Na Kuwa Ilikuwa Imeshaanza Kutuma Hapo Kabla. KatyCats Inasemekana Wako Tayari Kufa Ili Tu Katy Perry Aishi, Ni Mahaba Ya Hali Ya Juu Waliyonayo Katy Cat.
Arianators: Ariana Grande
Ukitaka Kujua Nguvu Ya Arianators Basi Waulize Twitter, Toka Alipotoa Ngoma Yake Ya The Way, Arianator Wamekuwa Na Nguvu Kubwa Sana Katika Kumpa Support Star Wao. Manchester Tragedy Ni Moja Ya Matukio Yaliomuonyesha Ariana Ni Namna Gani Anawapenda Mashabiki Wake. Arianator Wenyewe Wanaamini Siyo Mashabiki Wa Ariana Grande Bali Wao Ni Wapenzi Wa Ariana Grande
Kwa Leo Tuishie Hapo Next Time Tutaendelea Kuangalia Majina Ya Fanbase Mbalimbali Katika Ulimwengu Wa Burudani. Lakini Pia Unaweza Kutuachia Comment Hapo Chini Jina La Star Unayetaka Kujua Fanbase Yake.
0 comments:
Post a Comment