Je, Ni Bifu Au Ni Kiki, Bado Hatujajua, Lakini Ikumbukwe Kuwa Hakuna Kardashian Hata Mmoja Aliyewahi Kuwapongeza Rob Na Chyna Walipotangaza Kuvishana Pete Ya Uchumba.
Khloe Kaamua Kufunguka Hasa Kuhusu Uhusiano Wa Kaka Yake Na Chyna. Katika Kipindi Cha Keep Up With The Kardashian Khloe Alisikika Awambia Kim, Kourtney na Kylie Kuwa Hakuna Kuwapongeza Rob Na Chyna Kwa Hatua Hiyo Waliyoamua.
Khloe Alisema "Hatutakiwi Kuwapongeza, Kwani Najua Hayo Ni Maigizo Tu Na Naamini Mmoja Wao Ataachika Tu" Alisikika Khloe.
Katika Mzungumzo Hayo Kylie Naye Alisikika Akiwaambia Kuwa Tyga Ameshatweet Kuhusu Engagement, Kim Aliuliza Kwa Mshangao "Says What???
Kylie Akasoma Kile Alichokiandika Tyga "Kila Mtu Anahitaji Kuwa Na Furaha, Kile Watu Wanachofanya Ili Kuwapa Furaha Mimi Hayanihusu, Ilimradi Tu Haviingilia Furaha Yangu" Alimaliza Kusoma Kylie Ujumbe Huo Kutoka Kwa Tyga
Katika Kuunga Mkono Hoja Ya Khloe, Kylie Alisema "Nafikiri Dunia Inaweza Kudhani Labda Sisi Tunajali Sana, Lakini Ukweli Ni Kuwa Hakuna Anayejali Tunachotaka Ni Rob Mwenyewe Atuambie Kama Ameamua Kufanya Maamuzi Makubwa Kama Haya"
0 comments:
Post a Comment