Muziki Wa Hip Hop Na R&B Umetoka Mbali Sana. Na Hauwezi Kuzungumzia Muziki Huu Bila Kutaja Nguli Waliofanya Kazi Usiku Na Mchana Kuhakikisha Muziki Huu Unakuwa Hapa Ulipo Katika Dunia Hii Ya Burudani.
Mwaka Jana Mwezi Wa Kumi Channel Maarufu Kwa Burudani Duniani 'BET' Ilitoa Taarifa Za Kuaandaa A Reality Series Itakayoanza Kurushwa Mwezi June Mwaka Huu. Na Sasa BET Wanakwambia Kuwa Mambo Yameiva Kwani June 28 Mzigo Utaanza Kuonekana.
BET Wamewataja Nguli Wa Muziki Duniani Jermaine Dupri, Snoop Dog, Dame Dash Na Birdam Kama Main Character Wa Reality Series Hiyo.
Show Hiyo Itahusisha Maisha Ya Kila Siku Ya Mastaa Hao Kuanzia Namna Wanavyopiga Hela, Wanavyoishi Na Familia Zao, Mishe Zao Za Kila Siku Ziko Vipi Na Namna Wanavyopambana Na Changamoto Zinazowakabili.
Unaifahamu So So Def Ya Jermaine Dupri, Roc A Fella Record Ya Dame Dash, Cash Money Ya Birdamn Zote Hizi Zitakuwa Ndani Namna Zinavyojiendesha. Uhusiano Wa Cash Money Na Rich Gang Nao Utaujua Kupitia Show Hiyo.
Hii Siyo Show Ya Kukosa Kabisa Kutoka Kituo Chako Cha BET Save The Date Ni Tarehe 28/6/2016 Show Itaanza Kuruka Hewani.

0 comments:
Post a Comment