Eneo Maarufu Kwa Mastaa Wa Marekani Kuishi Linazidi Kunoga Baada Ya Mwanamziki Adele Kubisha Hodi Katika Eneo Hilo.
Panaitwa Beverly Hills, Huko Utakutana Na Mastaa Kama Jennifer Lawrence, Ashton Kutcher, Mila Kunis, Cameron Diaz, Nicole Richie Na Wengine Kibao.
Adele Inasemekana Ametoa Dolar 9.5 Milioni Ili Kuweza Kupata Eneo Hilo Lenye Ukubwa Wa Square Meter 631. Jumba Hilo Lina Vyumba Vinne Vya Kulala, Mabafu Sita Na Bwawa Kubwa La Kuogelea
Mpaka Sasa Adele Bado Hajaamia Katika Jumba Hilo Alilolinunua Mwezi Wa Nne Na Hii Ni Sababu Bado Yupo Kwenye Ziara Yake Ya Muziki.

0 comments:
Post a Comment