Sports

MOURINHO RASMI MANCHESTER UNITED

Kocha Mwenye Mbwembwe Nyingi Na Staili Ya Namna Yake Hasa Anapokuwa Uwanjani Jose Mourinho Amesaini Rasmi Kukinoa Kikosi Cha Manchester United.


Habari Kutoka Ndani Ya Klabu Hiyo Zinasema Kuwa Mourihno Amesaini Mkataba Wa Kukinoa Kikosi Hicho Katika Hoteli Ya Central London, Siku Ya Alhamisi Tarehe 26/5/2016.

Taarifa Za Kusaini Kwa Kocha Huyo Raia Wa Ureno Zimeokelewa Kwa Shangwe Kwa Baadhi ya Mashabiki Wa Timu Hiyo Yenye Maskani Yake Katika Viunga Vya Old Trafford Jiji La Manchester.

“Kuwa Meneja wa Manchester United ni heshima kubwa . Ni Klabu inayofahamika na kupendwa duniani kote” amesema Jose

Moja Ya Waliofurahia Kuja Kwa Kocha Huyo Ni Mchezaji Wa Zamani Wa Manchester United Rio Ferdinand Amabaye Anaamini Man Utd Inamhitaji Mourihno Zaidi Kwa Kipindi Hiki Ili Aweze Kurudisha Makali Yake Ya Zamani

Taarifa Zinasema Mourihno Amekubali Kusaini Mkataba Wa Miaka Mitatu Katika Klabu Hiyo ya Manchester United.

Tazama Video Fupi Ya Mourinho Akitambulishwa Baada Ya Kusaini Mkataba Wa Kufundisha Kikosi Cha Man UTD

About TNZ: Entertainment News

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.