Series

Series Zilizopigwa Chini: The Catch Na Scandal Ndani


Katika Habari Ambazo Wapenzi Wa Series Wamekuwa Wakizichukia Basi Ni Kama Hizi. Hakuna Kitu Kinauma Kama Kuona Series Yako Pendwa Imewekwa Juu Ya Mawe.

Kumekuwa Na Mijadala Mingi Juu Ya Sababu Za Series Kupigwa Chini Lakini Kila Mmoja Amekuwa Na Majibu Yake Japo Wengi Wamekubaliana Moja Ya Sababu Kubwa Ni Viewers Rate. Japo Kuna Wengine Walienda Mbali Na Kusema Inawezekana Series Nyingine Zinagusa Ukweli Juu Ya Yanayofanyika Katika Jamii Husika Mpaka Kutishia Uhai wa Usalama Wa Nchi.

Tumekuwa Baadhi Ya Series Ambazo Zimepigwa Chini Mpaka Sasa..

1. The Blacklist Redemption

Ilianza Kuruka Hewani Tarehe 23/2/2017 Na Ikarushwa Kwa Epsode 8 Ambapo Tarehe 13/4/2017 Epsode Ya Mwisho Ya Season One Ikarushwa. Wakati Tukisubiri Lini Season Two Itaruka Tunapata Taarifa Kuwa Imepigwa Chini.

2. The Catch

Baada Ya Kutoka Season Mbili Zenye Jumla Ya Epsodes 10 Kila Moja Waandaaji Pamoja Na ABC Wamekubaliana Kuiweka Pembeni Series Hii Iliyokuwa Inapendwa Na Wengi.

3. American Crime

Baada Ya Kukamilika Kwa Season 4 Usitarajie Tena Kuiona Hii, ABC Wameshaiweka Store Tayari Kwa Kupigwa Chini.

4. Secret n Lies

Baada ya Kushuhudia Purukushani Za Aina Yake Kwenye Series Hii Pendwa, Ilipotea Baada Ya Season 1 Lakini Wakaileta Kivingine Katika Season 2, Ila Sasa Wametuletea Taarifa Kuwa Tulipoangalia Mpaka Sasa Inatosha Hivyo Hawatairudisha tena.

5. APB

Baada ya Kutuonjesha Kwa Episodes 12 Za Season One, FOX Wametuletea Habari Kuwa Na Hii Tusitegemee Kuendelea Kuruka Hewani.

6.Scandal

Mpaka Sasa Zimesharuka Season 6, Na Bado Iko Moto, Lakini Sasa Kina Jini Mkata Kamba (ABC) Wanasema Kuwa Season 7 Itakuwa Ya Mwisho Kwa Scandal Kuruka. A Very Sad News.

7. Sleepy Hollow
Alifariki Miaka Za 100 Iliyopita Huko Uingereza, Akafufukia Katika Mji Wa Sleepy Hollow Akatupa Burudani Ya Aina Yake Kwa Series Yenye Season Nne Mfulululizo Sasa FOX Wameamua Kumuua Tena. Baada Ya Season Nne Za Kuvutia Sleepy Hollow Na Yenyewe Inasepa Kulala.

8. Emerald City
Burudani Ya Season Moja Tu, Imeonekana Inatosha Na Sasa Wanaenda Kupumzika Baada Ya Purukushani Za Emerald City

Zingine Ni Aftermath, Rosewood, Two Broke Girls, Frequency, No Tomorrow, Pitch, Incorporated, Outsiders, Man Seeking Woman, Doubt, Mercy Street, Girl Meets World, Good Girls Revolt, Blunt Talk, Brain Dead, Aquarius na Bates Motel.

Vipi Ulikuwa Unaifatilia Na Ipo Kwenye List Imekuuma Sana Kupigwa Chini.

Pia Kama Kuna Uliyofurahi Kupigwa Chini Hebu Tupe Maoni Yako Hapa Chini.

About TNZ: Entertainment News

2 comments:

  1. Sleepy horror na yenyewe inasepa kulala !!! ������

    ReplyDelete
  2. Dah sleepy horror ukiweza eka link ya season 3 & 4

    ReplyDelete

Powered by Blogger.