Celebrity

Muhammad Ali: Mshumaa Uliozima Ghafla Katikati Ya Kiza Totoro


Aliwahi Kuingia Matatani Mara Baada ya Kukataa Kwenda Kujiunga Na Jeshi la Marekani Vitani, Alishtakiwa na Misukosuko Kadhaa Ikampata


Katika Eneo La Kentucky Mwaka 1942 Mwezi Januari Tarehe 17 Ndiyo Alizaliwa Na Kupewa Jina La Cassius Marcellus Clay. Mwaka 1964 Alijiunga Na Uislamu, Na Kubadili Jina Lake Na Kuwa Muhammad Ali. Alisema: Aliamini Kuwa “Muhammad Ali ni Jina La Mtu Huru, Likimaanisha Kipenzi Cha Mwenyezi Mungu, Alisisita Na Kuwaomba Watu Walitumie Jina Hili Popote Watakapotaka Kuzungumza Na Yeye Au Hata Kama Watakuwa Wanamzungumzia Yeye Basi Watumie Jina La Muhammad Ali.” 


Muhammad Alipokataa  Kujiunga nA jeshi la Marekani Katika Vita Dhidi Ya Vietnam, Alitengwa Na Wamarekani. Jamaa Ni Mpingaji Mwenye Bidii Ambaye Atakumbukwa Daima Kama Shujaa. Aliwahi Kusema Sababu Ya Kukataa Kujiunga Na Jeshi La Marekani Alisema “Kwanini Nivae Gwanda Na Kusafiri Kutoka Nyumbani Kwenda Kuangusha Mabomu Na Risasi Kwa Wavietnam na Wakati Kwa Wale Weusi wa Marekani Kule Lousville Wanatendwa Kama Mbwa Na Kunyimwa Haki Zao Za Kibinadam? Hapana, Sitaweza Kwenda Kokote Kusaidia Mauaji Na Kuchoma Nyumba Za Taifa Masikini Ili Kuendeleza Ubabe Wa Hawa Mabwana Wa Watumwa Kwa Watu Weusi Dunia Nzima. 


Kwa Kukataa Kwake Kujiunga Na Jeshi La Marekani Alihukumiwa Kifungo Cha Miaka Mitano Ila Alikaa Nje Kwa Dhamana. Pasipoti Yake Ikafungiwa, Pia Shirika la Ndondi Duniani (World Boxing Association) Likamvua Taji La Ubingwa Na Kumsimamisha Kupigana Miaka Mitatu Na Nusu. Lakini Muhammad Hakuteteleka Na Aliendelea Kusimamia Kile Anachokiamini. Alipohojiwa Na Gazeti La Sports Illustrated Muhammad Ali, “Naachia Ubingwa Wangu, Utajiri Wangu Na Hata Mustakabali Wangu Wa Maisha Ya Siku Zangu Za usoni. Watu Wengi Mashuhuri Walijaribiwa Na Mitihani Kutokana Na Imani Zao za kidini. Naamini Nikifaulu Mtihani Huu Nitatoka Upya Nikiwa Mwenye Nguvu Na Ujasiri Zaidi ” 


Ali Aliendelea Kwa Kusema “Nategemea Kwenda Mbali Kusaidia Kuweka Watu Huru Huko Vietnam Na Wakati Huohuo Wenzangu hapa [Wamarekani Weusi] Wanafanyiwa Unyama, Inauma Kweli. Ni Bora Niwape Habari Wote Wanaodhani Nimepoteza Mengi, Ukweli Ni Kuwa Nimeingiza Vingi Zaidi. Nina Amani Moyoni, Na Dhamiri Iliyowazi. Huwa Ninaamka Nikiwa Na Furaha Na Ninapokiendea Kitanda Huwa Na Uso Wa Furaha Na Hata Kama Wakinifunga, Basi Nitakwenda Gerezani Huku Nikiwa Na Furaha Pia.”



Muhammad Ali Ndiye Bingwa Wa Muda Wote Ndondi Duniani Na Daima Ataendelea Kuitwa "The Greatest" Kwani Alishinda Medali Ya Dhahabu Katika Michezo Ya Olimpiki Ya 1960 Huko Rome; Mshindi wa Taji la Glavu za Dhahabu la Kentucky Mara 6; mshindi wa Taji la Glavu za Dhahabu wa Taifa (National Golden Gloves), Mwaka 1996 Alichaguliwa Kuwasha Mwenge Wa Mashindano ya Olimpiki Huko Atlanta; Mwaka 1990 Aliingia Katika Orodha Ya Wanandondi Wa kukumbukwa Wa Kimataifa (International Boxing Hall of Fame), Ameshinda Mataji Matatu Ya Uzito Wa Juu Akimshinda Sonny Liston (1964), George Foreman (1974) na Leon Spinks (1978) Na Kuwa Mwanandondi Wa Kulipwa Pekee Kushinda Mataji Hayo Mara Tatu. Meneja Wake Wakati Huwa Anamuita GOAT- Likimanish ‘The Greatest Of All Time’ Mwaka 1999 Alichaguliwa Kuwa Mwanamichezo Wa Karne Na Kituo Cha Habari Cha Sports Illustrated na BBC




Tuzo Zingine Alizowahi Kupokea Ni Pamoja Na Tuzo Ya Jim Thorpe (Jim Thorpe Pro Sports Award, Lifetime Achievement) 1992; Tuzo ya the Essence, 1997, Tuzo ya Arthur Ashe kwa Msaada Wake kwa Wote, ESPN (Espy), 1997, Tuzo Ya Msaaada Kwa Uongozi wa Marekani (Service to America Leadership Achievement), Kutoka  Baraza la Taifa la Mfuko wa Waaindishi Habari (National Association of Broadcasters Foundation), 2001.


Tazama Hapa Moja Ya Pambano Bora Kabisa Katika Ulimwengu Wa Ndondi


Muhammad Ali Alikuwa  Anaishi Michigan Na Mke Wake Wa Nne, Yolanda Williams. Muhammad Ali Ana Watoto Tisa: Rasheedah, Jamilah, Maryam, Miya, Khalilah, Hana, Laila, Muhammad Jr na Asaad. 


Alipoulizwa Na George Plimpton  “Kipi Ungependa Watu Wakikumbuke Kwako Pale Utapokuwa Umekwenda?”


Muhammad Ali Alisema“Ningependa Waseme, Alichukua Vikombe Kadhaa Vya Upendo, Aichukua Kijiko Cha Uvumilivu, Kijiko Kimoja Cha Ukarimu, Painti Moja Ya Huruma (Galoni Moja Ina Painti 8). Kwati Moja ya Tabasamu (Kwati Sawa na Painti Mbili), Kiasi Kidigo Cha Kujali, Na Akakoroga Niya na Furaha, Akaongeza Imani Nyingi, Na Akachanganya Vizuri Mchanganyiko Wake, Na Akagawa Kwa Watu Wake Wote Katika Maisha Yake.


Alipambana Sana na Kifo. Mara kwa Mara Aliingia Hospitali Akiwa Hoi Na Hajitmbui Lakini Aliweza Kutoka Ikiwa Imara. Ulipofika Wakati Wake, Alipokwenda Hakurudi Tena.  Amezima Kama Mshumaa Tena Katikati Ya Kiza. Bado Dunia Ilihitaji Busara Zake, Bado Tulihitaji Kujifunza Vingi Kutoka Kwake.


Nenda Muhammad Ali Daima Utabaki Kuwa Shujaa Wetu, Uliyetupigania Utakumbuka Daima Hasa Kwa Ule Usemi Wako Wa Fly Like A Butterfly & Sting Like A Bee'  Hakika Wewe Ni Kipepeo Uliyekua Unang'ata Kama Nyuki

About TNZ: Entertainment News

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.