Series

GOSSIP GIRL - MOJA YA SERIES ILIYOWAHI KUNIFANYA MTUMWA

Yes Ni Moja Ya Series Ambayo Ilikuwa Hata Nikitaka Kwenda Toilet Nakasirika, Ni Series Iliyonifanya Nje Nisikuone Kuna Maana, No Chuo No Ku Hang Na Washkaji Na Raha Zaidi Kipindi Kile I Was Single, So Sikuwa Na Kubanwa Na Baby Baby.

Hii Ilitoka Ikiwa Na Season Sita Ambazo Zote Kwa Pamoja Zilikuwa Na Jumla Ya Episodes 121, Ilianza Kutoka September 19, 2007 Na Ilimalizika December 17, 2012. Ni Teen Drama, Maisha Ya Vijana Wa Humptoms Ambao Kwa Namna Moja Au Nyingine
Inaleta Na Myingiliano W Wazazi Wao Katika Ishu Zao. Ikielezea Maisha Ya Shule, Ya Mtaani Yaliyotawaliwa Na Visa Kadhaa Vya Mapenzi. Huku Masha Yao Mengine Yakiwa Ni Ya Siri Ila Yakitolewa Na Mtandao Maarufu Wa Gossip Girl Na Kufanya Wasiamini Wapi Palipokwenda Wrong.

Serena   Van Der Woodsen
Mhusika Mkuu Ni Serena   Van Der Woodsen, Mara Baada Ya Kupata Scandal Anaamua Kuondoka Katika Huo Mji, Ila Baada Ya Muda Anaamua Kutudi Na Hapo Ndipo Mwanzo Wa Series Hii, Akaona Hawezi Kukimbia Nyumbani, Kaamua Kurudi Na Kukabiliana Na Kila Litakalotokea Mbele Yake. Akiwa Hajatulia Kabisa Katika Ishu Za Mapenzi Akikutwa Na Kashfa Kadhaa.

Sehemu Kubwa Ni Mapenzi Katika Maisha Ya Kila Siku, Kwa Tamaduni Zao Kule Ni Vitu Vya Kawaida The Way Wanavyopokezana Ku Date, Ila Kwa Mazingira Ya Kwetu Utabaki Unashangaa Tu Na Usielewe wanaishi Vipi.

Main Cast Ni Blake Lively As Serena Van Der Woodsen, Penn Badgely As Dan Humphrey, Leighton Meester As Blair Waldorf, Chance Crawford As Nate Archibald, Ed Westwick As Chuck Bass, Taylor Momsen As Jenny Humphrey & Jessica Sezhor As Vanessa Abraham.

Kila Mtu Ana Historia Yake, Kila Mtu Ana Mvurugano Wake Kila mtu Ana Siri Zake, Kila Mtu Ana Ups & Downs Zake. Si Ya Kukosa Hii.

About TNZ: Entertainment News

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.